Rodgers Kola
Ligi Kuu

Kola tishio jipya kwa Onyango na Inonga

Sambaza....

Achana na mabishano kuhusu uwezo wa Fiston Kalala Mayele mwenye mabao kumi na mbili katika msimu wake wa kwanza mpaka sasa kuna huyu Rodgers Kola mshambuliaji aliejiunga na Azam Fc msimu huu pia.

Baada ya Zakaria Thabit msemaji wa Azam Fc kusema Mayele ni mshambuliaji wa kawaida tuu katika Ligi wengi walimshukia haswa mitanadaoni wakipinga hoja yake.

Hazikupita siku nyingi Mayele akakutana na Simba na kutiwa mfukoni na Mcongo mwenzake Inonga Baka na kupeleka kuzima mtetemo wake. Sasa ni zamu ya Mshambuliaji Kola aliyepo Azam Fc kwenye ileile timu ambayo msemaji wake alisema Mayele ni wa kawaida na kweli akadhibitiwa na Henock Inonga.

Katika mchezo wa leo tutegemee vita kubwa ya ubora katika maeneo mengi uwanjani lakini muhimu zaidi ni vita ya Rodgers Kola dhidi ya Inonga Baka. Sikiliza na tazama kwa makini jinsi  Tigana anvyouchambua uimara wa Kola na kumpa nafasi ya kufunga mbele ya mfupa uliomshinda Mayele.

YouTube player

Sambaza....