Ligi Kuu

Kuelekea Derby: Makocha wakataa kupoteza mchezo huo.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Watani wa jadi kati ya Simba Queens na Yanga Princess utakaopigwa kesho Jumatano saa kumi jioni katika uwanja wa Uhuru kocha mkuu wa Simba Queens amesema wamejiandaa kushinda mchezo wao huo.

Charles Lukula kocha mkuu wa klabu ya Simba amesema hawataki kupoteza uongozi wao wa Ligi maana malengo yao ni kwenda kushiriki tena Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo walishika nafasi ya nne msimu huu.

 

“Tunaenda kucheza mechi ya Derby kesho tukiwa tunaongoza Ligi na hatutaki kupoteza alama yoyote kwakuwa lengo letu ni kutwaa ubingwa ili tupate nafasi ya kushiriki michuano ya CECAFA na hatimae Ligi ya Mabingwa Afrika kama tulivyofanya msimu ulioisha,” alisema Lukula.

Simba Queeens wanakwenda kukutana na Yanga Princess wakiwa kileleni na alama 26 sawa na Fountain Gate lakini wao wakiwazidi magoli. Yanga Princess wao wapo nafasi ya nne wakiwa na alama zao 21. 

Blessings Nkor mshambuliaji wa Yanga Princess. akimuacha mlinzi wa Simba Queens

Nae kocha ya msaidizi wa Yanga Princess Fred Mbuna amesema wanashukuru wapo salama na wamejiandaa vyema matazamio yao makubwa yapo katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba Queens.

Fred Mbuna “Wachezaji wangu wapo salama na tumejiandaa vyema kupata ushindi katika mchezo wa kesho. Makosa yaliyotokea michezo ya awali tumesharekebisha, kwasasa sifikirii michezo iliyopota tunafocus na mchezo uliopo mbele yetu,” 

Jentrix Shikangwa mshambuliaji wa Simba Queens.

Kuelekea mchezo huo nyota wakuchungwa katika vilabu hivyo viwili ni washambuliaji wao ambao wapo katika kiwango bora mpaka sasa. Mshambuliaji Jentrix Shikangwa anaonekana kuwa tishio mbele ya walinzi wa Yanga kwani mpaka sasa ana mabao tisa katika michezo tisa aliyoshuka dimbani.

Kwa upande wa Yanga wao wataingia uwanjani huku tumaini lao kubwa likiwa kwa mshambuliaji wao Blessings Nkor mwenye mabao matano mpaka sasa. 

Sambaza....