Ligi Kuu

Kwa Yanga hii ubingwa upo palepale!

Sambaza....

Mashabiki na wapenzi wa Yanga ni kama wameingia mchecheto hivi baada ya timu yao kudondosha alama mfululizo na kutoka katika njia ya ushindi.

Wananchi hawajapata ushindi katika michezo mitatu mfululizo huku pia wakishindwa kupata kufunga bao hata moja katika michezo hiyo na kupelekea presha ya ubingwa kuanza kutawala kuanzia kwa mashabiki mpaka kwa wachezaji wa Yanga.

Simba baada ya kushuka dimbani na kupata alama tatu mbele ya Kagera Sugar sasa imebakiza alama nane pekee ili kuifikia Yanga huku ikiwa imesalia michezo sita tuu kwa Ligi kumalizika.

Tazama hapa jinsi mpwa Tigana Lukinja akipiga hesabu za ubingwa wa Yanga katika michezo sita pekee iliyobaki na jinsi ambavyo Yanga wanatakiwa wafanye kuelekea ubingwa walioupoteza mbele ya Simba kwa miaka minne.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.