Uhamisho

Leonardo: Si sahihi kuwaacha nyota wa PSG!

Sambaza....

Imethibitika nyota Edinson Cavani na Thiago Silva wataondoka Paris Saint-Germain msimu huu wa joto baada ya mikataba ya wakongwe hao wawili kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mkurugenzi wa michezo wa kilabu hiyo Leonardo amethibitisha Cavani 33, na Silva 35, wote ni mikataba yao inamalizika mnamo Juni lakini watabaki na kilabu hadi msimu utakapokamilika kikamilifu kwani PSG wako kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Nahodha wa PSG Thiago Silva

“Ilikuwa uamuzi mgumu kuchukua. [Thiago Silva na Edinson Cavani] ni wachezaji ambao wamekuwa na mchango kubwa kwenye historia ya Klabu hii.

Daima unajiuliza ikiwa unapaswa kuendelea na njia ile ile au ikiwa ni bora kuepusha hali ambayo umekaa kwa mwaka mmoja zaidi. Imekuwa safari nzuri kama hii, lakini tumefika mwisho. Tulilazimika kufanya uamuzi wa kimantiki, kwa suala la kifedha na pia kuzingatia kizazi kijacho cha wachezaji wanaokuja.” Leandro aliiambia Le Journal du Dimanche.

Mshambuliaji wa PSG Edson Cavani

Mkurugenzi huyo wa ufundi pia hakusita kuonyesha majuto yake kwa nyota hao ambao wote wawili walisajiliwa wakitokea katika Seria A nchini Italia. Edson Cavani alijiunga na PSG akitokea Napoli na Thiago Silva alitokea AC Milan

Leonardo “Labda ni uamuzi mbaya, sijui haukua wakati mzuri kabisa. Ligi ya Mabingwa bado iko kwenye ajenda na mipango ni kubaki kwenye michuano na wao (Cavani na Silva) hadi mwisho wa Agosti.”

Sambaza....