Mabingwa Ulaya

Man Utd iliyobadilika inakutana na FC Barcelona

Sambaza....

Ni wachezaji watatu tu bado wapo na klabu ya Man Utd wakati Fc Barcelona ikikutana na Man Utd jumatano hii ambao walikuwepo mara ya mwisho wakati Barcelona anaifunga Man utd 3-1 katika fainali za ligi ya mabingwa, na ni mmoja tu ambaye yupo kikosi cha kwanza.

Chris Smalling

Chriss Smalling ambaye sasa ni beki wa Man Utd mwenye namba ya kudumu siku hiyo alikuwa benchi, wakati kina Rio Ferdinand wakipata kazi nzito ya kupambana na Lionel Messi.

Antonio Valencia na Michael Carrick wao walikuwa uwanjani katika mchezo huo. Kwa sasa Valencia hatumiki sana katika kikosi cha Man Utd, huku pia Michael Carrick akiwa na majukumu katika benchi la ufundi.

Messi akifunga bao mbele ya Rio

Kwa upande wa Fc Barcelona waliopo hadi sasa ni Gerald Pique, Lionel Messi na Sergio Busquets ambao walikuwa kikosi cha kwanza, na watakuwepo.

Timu zote zimekuwa na wachezaji wapya wengi, Man Utd itakuwa na Marcus Rushford, Paul Pogba,   Martial na wengine wengi, huku Fc Barcelona wakiwa na Dembele pia.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.