Ligi Kuu

Manara awashukia mashabiki wa ‘mitandaoni’.

Sambaza....

Anaandika Msemaji wa Klabu ya Simba Sc, Haji Manara.


Salaam

…wakati mwingine najiuliza nini wanadaamu wanataka? hasa washabiki wa Mpira!!

Nimetalii kidogo kwenye magroup(makundi) machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp (mtandao) nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo (jana) wa goli moja dhidi ya Prisons!!

Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha (Patrick) haufai!!

Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu..hisabati 3×3 ni tisa tu..hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane

Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!

Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!

Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!

Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!

Hapo ndio Haji naonekana mtata..aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu
Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba..kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya team toka kwa makocha.

Ni lazma mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu

Leo tumecheza na team(timu) nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa cc(sisi) …na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi..unachukua muda kdogo..

Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa draft au Chess ya kina Kasparov na Karpov..inahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake..vinginevyo ni kufanya uchale tu

Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya..usifate mkumbo wa mitandaoni

Mwisho niwasihi tena na tena cc(sisi) washabiki kazi yetu ni mbili tu..support na Dua na Sala..mengine ni kujitafutia kisukari kama si Pepopunda!!

Usiku mwema

Mkata vimeo
De Le Boss


 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x