Marcel Kaheza Boniventure akiwa katika uzi Majimaji fc.
Ligi KuuUhamisho

Marcel Kaheza na SimbaSc kwisha habari!

Sambaza....

Mshambuliaji wa Majimaji Marcel Boniventure Kaheza “Rivaldo” mwenye mabao 13 katika VPL ni swala la muda tuu kupewa jezi ya Simba rasmi.

Mchezaji huyo wa zamani Simba ni kama anarudi nyumbani baada ya kukitumikia kikosi hicho alipokua kinda akiwa Simba B, kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Majimaji ilipopanda daraja na kuamua kujiunga nayo moja kwa moja baada ya mkataba wake kuisha.

Marcel Boniventure akikitumikia kikosi cha SimbaSc

Marcel alionekana akiwa Dar es salaam baada ya kutumiwa tiketi ya ndege na viongozi wa Simba ili kuja kumalizana nae tayari kabisa kuwatumikia msimu ujao. Huku ikisubiriwa dirisha lifinguliwe rasmi ili aweze kujiunga na klabu yake hiyo mpya.

Marcel Boniventure “Rivaldo” amesajiliwa kwa dau la milioni 50 huku mshahara wake huenda ukawa milioni 2 kwa mwezi kilisema chanzo cha habari. Japo pande zote mbili zimegoma kuthibitisha hilo kwa nyakati tofauti.

Marcel anarudi Simba akiwa tayari amekomaa na uzoefu pia hivyo anatarajiwa kuungana na kina John Bocco na Emmanuel Okwi kuunda safu ya ushambilliaji kwa Wekundu wa Msimbazi ambayo itakua na  mashindano mengi msimu ujao. Huku akitegemewa kuanza kazi katika michuano ya Sportpesa Super cup kama mambo yatakwenda sawa.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x