Sambaza....

Mashabiki wa klabu ya Lipuli fc kutoka Iringa, watafunga safari kutoka Iringa mpaka Dar és salaam ili kuisapoti timu yao katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Yanga. Lipuli ilifanikiwa kupunguza ukame wa magoli baada ya kuichabanga Mbao Fc nyumbani kwake bao 3-1.

Wakiongea na tovuti hii baadhi ya mashabiki wameitikia muitikio wa michango ambayo imeaandaliwa kuja kuisapoti timu yao Jijini Dar es salaam, kila shabiki anatakiwa kuchangia 30,000 nauli ya kwenda Dar na Kurudi Iringa, pia ikiwa ni sehemu ya hamasa pia kwa wakazi wa mji wa Iringa waishio Jiji Dar kuisapoti timu hiyo.

Bofya mechi kupata takwimu za timu zote

Ujumbe unaopita kwenye Makundi ya Kusapoti Lipuli

*NDUGU ZANGU TUMEONA TWENDE DAR KWA AJILI YA KUISHANGILIA TIMU YETU YA LIPULI FC DHIDI YA YANGA JUMANNE 30.10.2018 HIVYO KAMATI YETU YA LIGI NA MASHINDANO IMEONA KILA ANAYETAKA KWENDA ACHANGIE 30,000/=NAULI YA KWENDA NA KURUDI, TUTAONDOKA JUMATATU SAA KUMI NA MBILI JIONI*

Namba ya kutuma mchango ni Mpesa 0754 720103 Isome Edger Kifyoga


“Twende tukaisapoti Lipuli, sisi kama Wanapaluhengo wa Iringa tutakuja, na wale wa Dar mje tuwape nguvu vijana” Alinukuliwa mmoja wa mashabiki katika mitaa ya Miyomboni, Iringa.
Ujumbe kwa Mashabiki walio Dar es Salaam

Kwa wale mashabiki wote wa Lipuli fc waishio Dar. Kutakuwa na msafara wa mashabiki utakaoanzia Ubungo terminal kwa ajili ya kwenda kuipa sapoti timu yetu pendwa ya Lipuli fc. Tutaanza kukutana kuanzia saa sita kamili mchana na kuondoka kwenda uwanjani itakuwa saa kumi kamili. Usafiri wa kwenda na kurudi utakuwepo. UPATAPO HABARI HII MJULISHE NA MWENZIO. Nalunoge lweki.


Yanga hajapoteza mchezo hata mmoja katika kituo chake cha Dar es salaam, na anasare moja tu dhidi ya mtani wake Simba sc. Hakika inategemewa kuwa mchezo muhimu kwa pande mbili hizi.

Sambaza....