Mashindano

Mashemeji waibuka wababe Challenge Cup!

Sambaza....

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara  “Kilimanjaro Stars” imeanza michuano ya Challenge Cup nchini Uganda vibaya baada ya kupokea kipigo katika mchezo wao wakwanza.

Baada ya ndugu zao Zanzibar Heroes kutoka sare na Sudan katika  mchezo wa awali wa kundi B, Kili Stars imekubali kichapo kutoka kwa “mashemeji” Kenya cha bao kwa sifuri.

Bao la Kenya likifungwa mapema kabisa katika dakika ya 4 na Hassan Abdallah baada ya kupokea pasi safi na kumzidi ujanja Mohamed Hussein na kufanikiwa kuuweka mpira kimiani akipiga shuti kali na kumpita mlinda mlango Aishi Manula.

Licha mwalimu wa Kili Stars kufanya mabadiliko kadhaa ya kuwaingiza Eliuta Mpepo, Hassan Dilunga na Ditram Nchimbi lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na hivyo kupelekea kupoteza alama zote tatu.

Baada ya kupoteza mchezo huo sasa  Kilimanjaro Stars inajiandaa kupepetana na ndugu zao Zanzibar Heroes katika mchezo unaofuata.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.