Washambuliaji wa Yanga Crispine Ngushi (kushoto) na Fiston Mayele (kulia)
Ligi Kuu

Mayele alistahili kupiga penati.

Sambaza....

Baada ya Yanga kwenda suluhu katika michezo mitatu mfululizo tayari mashabiki wake wameanza kuonyesha hisia zao kutokana na matokeo hayo mabaya ya timu yao.

Ni kwa mara ya kwanza katika msimu huu Yanga imecheza michezo mitatu mfululizo bila kutoka na ushindi na bila kufunga bao lolote. Mbaya zaidi katika michezo yote mitatu Fiston Mayele mshambuliaji kiongozi wa Yanga alikuepo na alianza kikosi cha kwanza.

Joash Onyango akimdhibiti Fiston Mayele katika mchezo wa Derby ya Kariakoo ambayo iliisha kwa suluhu.

Katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Yanga walipata tuta baada ya Feisal Salum kufanyiwa madhambi katika eneo hatari. Djuma Shaban mpigaji penati namba moja wa Yanga alienda kuchukua mpira na kutaka kuupiga mkwaju wa penati lakini Saidoo alimpokonya mpira ule na kumpa Mayele, tazama hapa kilichotokea na jinsi Tigana Lukinja akilichambua tukio lile.

YouTube player

Sambaza....