Mataifa Afrika

Migne ataja 30 wa awali kwa ajili ya AFCON.

Sambaza....

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Kenya ‘Harambee Stars’ Sebastien Migne ametangaza majina ya awali ya wachezaji 30 kwa ajili ya michezo ya kirafiki kujiandaa na michuano ya Mataifa Afrika inayotazamiwa kufanyika kuanzia mwezi ujao nchini Misri.

Katika kikosi hicho kilichotangazwa leo, wachezaji 11 walioitwa wanacheza ligi za ndani huku wengine waliosalia wakicheza katika vilabu mbalimbali barani Afrika na Ulaya.

Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC na aliyefanya vizuri katika michuano ya SportPesa mwaka jana Allan Wanga ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Kakamega Homeboys ni miongoni mwa walioitwa kwenye kikosi hicho.

Makipa: Patrick Matasi (St. Georges, Ethiopia), Faruk Shikhalo (Bandari FC, Kenya), John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya), Brian Bwire (Kariobangi Sharks)

Walinzi: Philemon Otieno (Gor Mahia-Kenya), Musa Mohammed (Nkana FC-Zambia), Joash Onyango (Gor Mahia-Kenya), Abud Omar (Sepsi Sfântu-Romania), David Owino (Zesco United-Zambia), Bernard Ochieng (Vihiga United-Kenya), Brian Mandela (Maritzburg United-South Africa), Erick Ouma (Vasalund IF-Sweden), Joseph Okumu

Viungo: Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs-England), Anthony Akumu (Zesco United-Zambia), Eric Johanna (IF Bromma-Sweden), Ismael Gonzales (UD Las Palmas-Spain), Francis Kahata (Gor Mahia-Kenya), Dennis Odhiambo (Sofapaka FC-Kenya), Johanna Omollo (Cercle Brugge-Belgium), Christopher Mbamba (Oskarshamns AIK-Sweden), Whyvonne Isuza (AFC Leopards, Kenya), Clifton Miheso (Portugal)

Washambuliaji: Paul Were (AFC Leopards-Kenya), Ayub Timbe (Beijing Renhe-China), Michael Olunga (Kashiwa Reysol-Japan), Allan Wanga (Kakamega Homeboyz-Kenya), John Avire (Sofapaka), Masud Juma (Libya), Ochieng Ovella (IF Vasalund, Sweden).

Kenya ipo kundi moja pamoja na Tanzania kwenye kundi ambalo linaundwa na wababe wengine wa Afrika Senegal na Algeria na ratiba inaonesha kwamba Kenya wataanza kwa kuumana na Algeria Juni 23 kabla ya baadae kucheza na Tanzania Juni 27 mjini Cairo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.