Ligi Kuu

Mkude ni rekodi juu ya rekodi katika “Derby” ya Kariakoo

Sambaza....

Jonas Mkude ‘NunguNungu’ kama anavyoitwa kiungo mkabaji toka pale kwa Wanalunyasini diyo mchezaji anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi za kariakoo derby yaani michezo inayouhusisha Simba na Yanga akiwa amecheza michezo 22 na anatarajiwa kucheza mchezo ya 23 jumamosi hii.

Haikuwa rahisi kijana huyu mtoto wa kinodoni kucheza michezo mingi ya derby hii lakini ukweli nyuma yake kuna siri kubwa iliyofichika.

Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba

Basi ni siri gani hiyo? ni uwepo wake Simba muda mrefu na kujiakikishia namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho kwa makocha wote waliowahi kufanya kazi na Simba tangu kijana huyo kupandishwa kikosi cha kwanza msimu wa 2012- 13 tangu hapo hajakosekana katika derby kama anautimamu wa afya.

Kwa rekodi ya pili ya kuwepo kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 10 unapata rekodi nyingine ndiye mchezaji pekee wa muda mrefu ndani ya derby ya Kariakoo akihudumu kwa hiyo miaka.

Jonas Gerad Mkude “Nungunungu”.

Pamoja na rekodi zake nyingi nzuri za kuvutia kwenye Derby ya kariakoo, Mkude hajawahi kufunga goli kwenye open game zaidi ya changamoto ya mikwaju ya penalty 5 kwa zile mechi zilizoamriwa na hatua hiyo.

Pia ni mhanga wa kadi nyekundu katika moja ya mechi za kariakoo derby pale Estadio de Mkapa Leo ananenda kutuendikia rekodi gani tusubiri tuone.

Sambaza....