Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee la Henock Inonga dhidi ya Vipers
Mabingwa Afrika

Mnyama afufukia Uganda!

Sambaza....

Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatimae wamefufuka na kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika Kundi C.

Goli pekee la Henock Inonga Baka limefanikiwa kuipa Simba alama tatu kwa kutoka na ushindi wa bao moja bila dhidi ya wenyeji wao Vipers katika Dimba lao la St Mary.

Goli la  Simba lilifungwa dakika ya 19 kupitia mpira wa adhabu uliopigwa kwa ustadi mkubwa na Mohamed Hussein Zimbwe aliekua nahodha katika mchezo wa leo.

Kwa ushindi huo sasa Simba inasogea mpaka nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu nyuma ya Raja na Horoya ambao wanakwenda kupepetana katika mchezo wa saa nne usiku.

Kwa ushindi huo sasa Simba wamefufua matuamini yao yakufuzu hatua ya robo fainali na sasa wanasubiri michezo miwili ya nyumbani dhidi ya Vipers na Horoya ili kujikusanyia alama sita kabla yakumaliza mchezo wamwisho ugenini dhidi ya Raja Casablanca.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Raja Casablanca atamkaribisha Horoya kutoka Guinea katika dimba la Mohamed VI mabapo Vipers alisuulubiwa kwa mabao matano kwa sifuri.

Sambaza....