Ligi KuuUhamisho

Mo Ibrahim kwenda Yanga kwa mkwanja mrefu!

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa Simba Mohamed Ibrahim “Mo” anakaribia kujiunga na Yanga sc akitokea kwa mahasimu wao  Simba sc mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wa Mo Ibra na Simba unaisha mwisho wa msimu huu hivyo yupo huru kuongea na timu yoyote inayotaka huduma yake. Na hivyo kuipa nafasi klabu ya Yanga  kuanza nae kufanya mazungumzo ya kumsajili kwajili ya msimu ujao.

Mo Ibra amesema yupo tayari kujiunga na klabu ya Yanga kwa dau la millioni 70 na kusaini kandarasi ya miaka miwili na mshahara wa millioni 2.

 

Klabu ya Yanga  imesema ipo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa ili kupata huduma yake lakini tatizo kubwa likibaki kwenye mshahara na kulipa hela ya usajili. Uongozi wa Yanga umekua ukihangaika kupata hela cash ya kumlipa kutokana na mchezaji mwenyewe kutokua tayari kupokea hela nusunusu.

Mo Ibra alikua na msimu mzuri mwaka wake wa kwanza alipojiunga na Simba akitokea Mtibwa sugar huku akifanikiwa kuipa ubingwa wa Azamsports Federation  Cup, kabla ya msimu huu kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya kocha mpya Mfaransa Piere Lenchentre.

Kiungo huyo wa zamani wa Mtibwa amekua hana maelewano mazuri na kocha mpya hivyo kumfanya akae benchi muda mrefu na hivyo kumfanya mchezaji huyo kufikiria kuondoka kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x