Ligi Kuu

Mshambuliaji arudi Polisi!

Sambaza....

Mshambuliaji wa Polisi Tanzania Vitalis Mayanga amerejea mazoezini baada ya kukaa nje ya uwanja muda mrefu kutokana na majeruhi ya kidole aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Simba.

Akizungumza tovuti ya Kandanda.co.tz msemaji wa klabu ya Polisi Tanzania Hassa Kayoza amethibitisha nyota wao huyo amerejea kikosini na tayari ameungana na wenzake.

Vitalis Mayanga

“Nakujulisha kurejea dimbani kwa kinara wetu wa magoli Vitalis Mayanga ambaye alikuwa nje ya uwanja tangu April 10 alipoumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba uwanja wa Ushirika,” Hassan Kayoza

“Mayanga alivunjika kidole cha mguu na kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya KCMC na kutakiwa kuwa nje kwa wiki sita,” alisema

Kayoza pia amethibitisha tayari Mayanga yupi kambini kujiandaa na michezo miwili iliyopo mbele yao dhidi ya Namungo Fc na Yanga.

“Vitalis Mayanga ameanza mazoezi leo asubuhi na wenzake katika shule ya maafisa wa Polisi (DPA) Kurasini. Hadi anaumia alikuwa ameshaifungia timu yetu magoli 6 katika michezo ya Ligi kuu ya NBC.” Kayoza msemaji wa Polisi Tanzania.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.