Wachezaji wa Simba wakishangilia mbele ya mashabiki wao
Ligi Kuu

Mshambuliaji wa Simba atabiri mechi yao na Yanga

Sambaza....

Kuelekea mechi ya Watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itakayopigwa siku ya Tarehe nane March mshambuliaji wa zamani wa Taifa Stars na Simba ameipa nafasi timu yake hiyo ya zamani kuibuka na matokeo ya ushindi.

Athumani Machupa mshambuliaji hatari wakati wa enzi zake alipokua anaitumikia Simba sc amesema Simba itaibuka mshindi katika mchezo huo huku pia akitaja na idadi ya magoli.

Athumani Machupa “Mtazamo wangu bwana katika mchezo wa Jumapili matokeo ni mabao mawili kwa sifuri, sio kwa unazi lakini Simba itashinda. Mimi naona  ni hivyo na hii ni  kutokana na vikosi hivyo vya timu zote mbili kwa jinsi ninavyoviona.”


Yanga SC vs Simba SC


Machupa pia aliongelea hali ya mchezo na form ya timu zote mbili huku akizungumzia mchezaji mmoja kwa mmoja.

Machupa “Yanga anakufa mwandishi,  “tention” ya mechi kwa timu zote ipo wazi na unaona ni nani yuko sawa. Pia hata uzuri wa mchezaji mmoja mmoja Simba bado iko vizuri, japo mechi hizi huwa ngumu sana na kutoa matokeo ya kushangaza.”

**Kabla ya mechi za mzunguko wa 25 na 26 Ligi Kuu

Wakati aa enzi zake Athumani Machupa alikua mshambuliaji hatari akiitumikia Simba huku akiwa na muunganiko wa hatari na Emmanuel Gabriel Mwakyusa “Batgol”.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.