Harrison Mwakyembe waziri mwenye dhamana ya michezo!
Ligi Kuu

Mwakyembe amtaja Molinga, alisifia jeshi!

Sambaza....

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amezungumaza na kituo cha redio cha Efm katika kipindi cha michezo na kuweka wazi jinsi alivyomuulizia nyota wa DR Congo David Molinga.

Katika mchezo uliowakutanisha JKT Tanzania dhidi ya Yanga katika dimba la Jamuhuri Dodoma Jumatano June 17 ambapo matokeo yalikua sare kwa bao moja kwa moja, Mh. Mwakyembe alikuepo uwanjani hapo kuushuhudia.

Yanga sc vs JKT Tanzania
Mwakyembe amesema:”Unajua timu za jeshi hazina mapumziko, wao kipindi cha Corona hakuna Corona lazima wawe fiti kwa kufanya mazoezi sasa nilishangaa nilipoona kikosi cha Yanga hakina Molinga.
“Niliwauliza wale ambao nilikuwa nao, jamani mbona Molinga hapa simuoni akianza ila baadaye kidogo nilimuona akiingia, wale ni wanajeshi lazima kikosi kitakachopambana nao kiwe na nguvu muda wote.”
David Molinga “Falcao”.
Katika mchezo huo JKT ndio waliokuwa wakwanza kupata bao kupitia kwa Michael Aidan kabla ya Patrick Sibomana kusawazisha kipindi cha pili. Pia ilishuhudiwa vurugu kubwa mchezo ulipokua unaelekea mwishoni na kupelekea Mwinyi Kazimoto na Lamine Moro kuonyeshwa kadi nyekundu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.