Ligi Kuu

Namungo Fc 1- 1 Yanga, Tunalipwa kesho

Sambaza....

Matokeo fair kwa kila timu kwa jinsi zilivyocheza, japo mapungufu ya kiamuzi yameufanya mchezo umalizike kwa sare.
Yap! Hii ndiyo Yanga. Wenyewe wanaposema Daima mbele nyuma mwiko huwa wanamaanisha. Kukosa kundi kubwa la wachezaji muhimu kisha ukaondoka na alama 1 katika kiwanja kigumu cha Majaliwa Stadium sio kazi nyepesi. Ni kazi ngumu iliyozishinda timu nyingi. Welldone kwao .

Deus Kaseke angeweza kuifanya Yanga iondoke na pointi zote tatu na tukamtaja kama shujaa wa mechi, lakini kushindwa kuusoma mchezo na kujipanga vyema tumefanya tumshangae zaidi yeye aliyeingia dakika 20 za mwisho kuliko kuwashangaa kina Morrison walioanza mechi.


1 - 1
Uwanja wa Majaliwa

Namungo FC vs Yanga SC


Unapokuwa mchezaji wa timu ya daraja la Yanga unatakiwa kuwa active muda wote mchezoni. Kuna sehemu alitakiwa kuwepo hakuwepo, kuna sehemu alitakiwa kuuchukua mpira na kumpasia mwenzake afunge hakuwepo. Dakika zake 20 zinatosha kuonyesha msimu ujao anastahili kuwa mchezaji wa timu gani .
Deus Kaseke
Bado niko na Kaseke. Anapaswa kujiuliza inakuwaje Morrison mwenye majeraha anakuwa mchezaji hatari, yeye mzima hana madhara? Ni swali analopaswa kujiuliza.
Kikoti hakuwa katika kiwango chake bora leo, lakini ile pasi yake kwa Blaise Bigilimana aliyesawazisha bao inamfanya kuwa miongoni mwa mashujaa wa mechi hii.
George Makang’a, Hassan Manyanya walikuwa bora kwa baadhi ya mikimbio yao kiwanjani, lakini ‘ndoa’ ya Tshithimbi na Feisal pale kati imefanya vijana wasiwe na madhara sana katika lango la Yanga.
Ni wakati wa wachezaji wetu kuanza kujifunza kucheza kwa filimbi na kusimamisha mchezo kwa filimbi. Kama hujasikia filimbi endelea kucheza. Kina Makapu wangeweza kumfikia Blaise na kuuokoa mpira, lakini hii kusubiria mpaka filimbi ipigwe ndiyo waanze kucheza imeshaonekana ni kama changamoto kwa waamuzi wetu. Wachezaji wajifunze hili.
Tunalipwa kesho

Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.