Ligi Kuu

Nashusha bonge la mjengo Dodoma- ZAHERA

Sambaza....

 

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera anataka kupafanya Tanzania kama nyumbani kwake baada ya Congo .

Kocha huyo amedai kuwa ana mpango wa kujenga nyumba katika mji wa Dodoma ndiyo maana anatumia muda mwingi pia kuwepo Tanzania mara baada ya kuachana na Yanga .

Kocha huyo amedai kuwa pamoja na kwamba yuko Tanzania kushughulikia Madai yake na Yanga Lakini pia yuko anashughulikia ujenzi wa nyumba yake kule Dodoma.

“Nilipewa uwanja na yule mama kule Dodoma , Kwa hiyo nipo nashughulikia ujenzi wa nyumba yangu kwenye uwanja niliopewa kama zawadi na yule mama kule Dodoma “- alimalizia kocha huyo wa zamani wa Yanga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.