Ligi Kuu

Ndugai mgeni Rasmi, mechi ya Simba na Yanga.

Sambaza....

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara utakaowakutanisha watani wa Jadi Simba na Yanga kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumapili hii.

Ndugai atashuhudia mchezo huo wa kwanza kwa msimu huu kuwakutanisha Simba na Yanga, na mechi ya tatu kwa umaarufu Barani Afrika ikitanguliwa na mechi kati ya Zamaleki na Al Ahly kule nchini Misri na ya pili ni mahasimu wakubwa wa ukanda wa SADC, Kaizer Chiefs na Orlando Pirate almaarufu kama Soweto derby.

Tayari waamuzi wa mchezo huo wamekwisha kutangazwa na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Mwanadada Jonesia Rukya akisaidiwa na na Frednand Chacha na Mohamed Mkono huku mwamuzi wa akiba akiwa Elly Sassi kutoka Dar es Salaam.

Mpaka kuelekea kwenye mchezo huo Yanga ambao watakuwa wageni, wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 12 huku Mnyama Simba Sports Club wao wakiwa katika nafasi ya sita baada ya kushuka dimbani mara tano na kukusanya alama 10.

Sambaza....