Ligi Kuu

Ni vita isiyoumiza, Wawa vs Nchimbi?

Sambaza....

Paswal Wawa alikua na shughuli pevu ya kumuonjesha joto ya jiwe mshambuliaji mpya wa Yanga sc Ditram Nchimbi katika mchezo wa Watani uliomalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Nchimbi akiwa ndio mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya Yanga na pia mchezo wa kwanza wa Watani alionjeshwa joto hilo na beki mzoefu Pascal Wawa, katika dakika 90 za mchezo huo.

 

Pascal Wawa alimfanyia vurugu isiyoumiza Nchimbi na kufanikiwa kummbana kwa dakika zote za mchezo na kifanikiwa kumdhibiti asifunge wala kutoa pasi ya bao.

Pascal Wawa akimkanyaga Ditram Nchimbi

Lakini pia Pascal Wawa akionekana kimfanyia vitendo visivyo vya kiungwana akionekana akimkanyaga Ditram Nchimbi akiwa kwenye harakati za kumdhibiti akiwa nje ya uwanja baada ya kumuangusha katika haraki za kumdhibiti asilete madhara langoli kwa Simba .

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.