Sambaza....

Kocha wa timu ya soka ya Mbeya City ‘Wanakomakumwanya’ Ramadhan Nswanzurimo amesema hatoangalia rekodi ama michezo iliyopita watakapokwenda kucheza na Yanga siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Aidha Nswanzurimo amesema wanafahamu Yanga ni timu ambayo inaweza kuamua matokeo kwa namna yoyote ile katika mchezo hivyo wamezidi kujiandaa kiphiziki na kisaikolojia Ili kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo.

“Kama Kuna mchezo tuliwazuia na kupata sare hiyo tayari imepita, tumejiandaa na mchezo wa Jumamosi, Yanga ni timu nzuri, wapo na wachezaji wanaoweza kuamua matokeo, timu Kama timu unaweza ukawazuia lakini wakipata set piss moja, Kuna wachezaji wanaocheza set piss Vizuri na wanapata matokeo,”.

“So vipo vitu vingi ambavyo tumejiandaa navyo, tumejitayarisha Saikolojia ipo vizuri kwa maana ukicheza na timu kama Yanga vipo vitu vingi vinachezeka na kutokea hata nje ya uwanja, vinavyoweza kubadilisha matokeo uwanjani, Ila tupo tayari tunawasubiri tu hapa Jumamosi,” amesema.

Mbeya City watakuwa wenyeji wa Vinara Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya Jumamosi hii.

Sambaza....