Ligi Kuu

Ongala alimpa mpira Mgunda akachagua njia yake.

Sambaza....

Kalimangonga Ongala anafanikiwa kuiongoza Azam Fc kupata ushindi mbele ya Simba ya Juma Mgunda baada ya Azam Fc kusota bila ushindi kwa michezo kumi mfululizo katika michezo ya Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo huo uliofanyika katika Dimba la Benjamin Mkapa badala ya Chamanzi kama ambavyo awali ulipaswa kupigwa Azam walikua katika ubora mkubwa wa kimbinu tofauti na wapinzani wao Simba na kupelekea kupata ushindi wa bao moja bila lililofungwa na Prince Dube.

Ongalla aliamua kuweza wachezaji wengi eneo la katikati mwa uwanja huku mara nyingi wakikaa chini na kuwasubiri Simba washambulie huku yeye akifanya mashambulizi yakushtukiza kupitia pembeni mwa uwanja akitumia kasi za Kipre Jnr na Ayoub Lyanga.

Kipre Jnr akianguka mbele ya walinzi wa Simba Joash Onyango na Inonga Baka

Tangu Simba iwe chini ya Juma Mgunda imekua ikishambulia na kupata mabao yake mengi kwa kutumia kasi za Mosses Phiri, Augistine na ufundi wa Clatous Chama. Mgunda amekua akichanga karata zake vyema pale ambapo mpinzani anapopoteza mpira na kushambulia haraka kabla ya mpinzani hajakaa katika “shape” yao nzuri ya kuzuia.

Simba wamekua wakifunga mabao mengi kwa kuwaacha wapinzani wachezee mpira halafu wakifanya “pressings” na wakipokonya mpira hufanya mashambulizi ya haraka na kuufikia ukuta wa timu pinzani mapema. Hii mara nyingi hutegemea kasi za kina Phiri, Okrah ama Chama.

Rejea magoli ya Simba waliyoyafunga Angola dhidi ya Agosto, pia katika mchezo dhidi ya Yanga bao la Augustine Okra lilipatikana kwa kupigwa pasi tano tu.

Augustine Okrah akifunga mbele ya mlinda mlango wa Yanga Augustine Okrah

Kally Ongala alifanya “home work” kwa usahihi zaidi na kuliona hili hivyo akaamua kuwaacha Simba wacheze mpira na wao kurudi nyuma. Hii iliwapa ugumu Simba kwani kila wakijenga mashambulizi wanawakuta Azam Fc wapo katika “shape” yao ileile ya ulinzi na kuwawia ugumu kutengeneza nafasi za mabao.

Azam waliifunga Simba bila tabu kabisa baada ya Kally Ongala kumpa mpira Mgunda na kumuacha auchezee huku yeye akirudi nyuma na kubaki katika shape yake ileile ya ulinzi. Shukrani kwa juhudi binafsi za Prince Dube alietumia uwezo binafsi na makosa ya Erasto Nyoni yakutokua katika nafasi yake kufunga bao lililoamua mchezo na kuhitimisha vyema mbinu za Kali Ongalla.

 

 

Sambaza....