Pablo Franco
Ligi Kuu

Pablo anastahili lawama za John Bocco

Sambaza....

Kupungua kwa makali ya safu ya ushambuliaji wa Simba chini ya nahodha John Bocco, Meddie Kagere na Chriss Mugalu Pablo hawezi kukwepa lawama hizi.

Utatu huu wa Simba ya msimu uliyopita ilimaliza na jumla ya magoli 44 kati ya mabao 78 yaliyowapa wekundu hao wa msimbazi ubingwa.

John Bocco akiwa mfungaji bora alifunga (16) Chriss Mugalu (15) na Meddie Kagere (13)
na kufanya kwa umoja wao kifikisha juu ya nusu ya magoli yaliyowapa ubingwa huo.

John Bocco.

Msimu huu ni hali tofauti sana tena sana tu, mpaka wakati uliopo jumla ya magoli yao yote kwa hiyo ‘trio’ ni 8 tu na tumebakiza mechi 8 kumaliza msimu.

John Bocco alifunga goli lake la kwanza katika mchezo dhidi ya Ruvu na kwenda kuungana na yale 7 aliyonayo Kagere na kufanya uliokuwa ‘Utatu mtakatifu ‘ kuwa na magoli hayo 8.

Pablo hakwepi lawama hiyo hata kidogo nionavyo mimi, yeye ndiyo Kocha mkuu ambayo vitu vyote vya kiufundi kama havitoki kwake basi anavihalalisha kwenye matumizi.

Pablo Franco.

Swali la kwanza ni aina ya training anayowapa hasa kwenye ‘finishing skills’ anawapa mara ngapi kwa wiki!?

Lakini pili filosofi yake ya ufungaji inategemea nini? Krosi au pasi mpenyezo ( Penetrations), je wajibu huu unatimizwa kuna kross za kutosha ndani ya mechi, kuna pasi za kutosha za kupenyeza, Mobility na interchange zinafanyika na washambuliaji?.

Ni imani yangu kuna kitu kinakosekana kwenye eneo la ufundi kutoka kwa Kocha hii inaweza kuchangiwa na nafasi aliyocheza Pablo kwenye Career yake.

Yusuph Mhilu akipiga shuti mbele ya mlinzi wa Namungo Abdulmalick Zakaria.

Kwa nyogeza ya hili ni kwamba hata sajili mpya kama Yusuph Mhilu naye ameangukia kwenye mporomoka huu licha ya kuja na bao 9 akitokea Kagera Sugar hadi sasa hajafunga goli lolote katika Ligi.

Kibu Denis aliyekuja na magoli 6 akitokea Mbeya City ndiye pekee anayeonekana kufanikiwa kwani hadi hivi sasa ana mabao 5.

Kwa mantiki hiyo unaona kuwa ‘trio’ hiyo ya Simba inadeni la angalau goli 14 kwa pamoja ili angalau kufikisha nusu ya goli hizo 44 walizozifunga msimu ulio pia huku kukiwa kumesalia mechi 8 hili linawezekana?

Sambaza....