Papy Kabamba Tshishimbi.
Blog

Papy Tshishimbi ana nafasi kikosi cha Simba- Haji Manara

Sambaza....

Mkuu wa kitengo cha habari cha Simba Sports Club Hajji Manara amekiri Papy Kabamba ni moja viungo anaowakubali katika ligi  huku akisema ni aina ya viungo wa zamani wanaocheza sasa mpira katika zama hizi.

Haji hakusita kusifia kujituma na kucheza nafasi zaidi ya moja kwa Mcongo huyo ambae mpaka sasa hajasaini kandarasi mpya na timu yake ya Yanga, mkataba wa Papy na Yanga unaelekea ukingoni ikiwa imebaki miezi miezi michache umalizike.

Manara Papy ni “box to box midfileder” bora kuwahi kumshuhudia katika zama hizi, ni kiungo mwenye uwezo wa hali ya juu. Hata akija pale Simba anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza moja kwa moja.

Manahodha wawili walipokutana, huku Papy akimuonyesha kazi Tshabalala

Uzuri wa Papy anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja anacheza namba 6 namba 8 hata mwalimu akiamua kumuweka “ribero” atacheza vizuri tuu. Ni moja ya wachezaji ninaowahusudu, lakini simaanishi kua Simba tunataka kumsajili hapana, namuongelea tuu kama mchezaji mzuri lakini msihusishe na kutaka kumsajili katika timu yetu.”

Manara amesema Papy ndie mchezaji pekee mwenye uwezo wa kucheza Simba akitokea Yanga na kusema hata mashabiki wa Yanga wanajua hilo na wanatamani wachezaji wa Simba wangekua ni wao.

Manara “Ukianzia golini Manula ni zaidi ya Menata, Kapombe bora zaidi ya Juma Abdul, Tshabalala ni ziad ya Japhary, labda wachezaji wawili tuu wa Yanga wanaweza kuingia katika kikosi cha Simba. Hata yule Morrison akija Simba ni lazima aanze kwanza kugombania nafasi na wachezaji wengine.”

Japhary Mohamed akipambana na Shomari Kapombe

Kumekua na tetesi za Simba kuitaka saini ya Papy Kabamba Tshishimbi ambae kwasasa ndie nahodha wa Yanga, huku Yanga nao wakihaha kutaka kumbakisha kikosini Mkongo huyo.

Manara alimzungumzia Papy baada ya kuulizwa na mtangazaji wa redio ya East Africa akiwa katika kipindi cha kipyenga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.