Kocha wa Simba Sc, Aussems
Tetesi

Patrick Aussems kurudi SIMBA

Sambaza....

Kelele za mashabiki wa Simba kumtaka Patrick Aussems hazikuishia kwenye uwanja wa uhuru tu pale jana , inavyoonekana zimeenda mbali zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii.

Mashabiki wa Simba wamemfuata kwa wingi kocha wao wa zamani Patrick Aussems kumtaka arudi tena kwenye timu yao baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao kwa sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kocha huyo wa zamani wa Simba amedai kuwa anashukuru kuona mashabiki wakituma sms nyingi wakimtaka arudi tena.

Amedai kuwa amepokea jumbe nyingi zikimtaka arudi Simba , anashukuru kwa hilo na anaamini kuwa Simba ni timu kubwa na yenye mashabiki wazuri na anawatakiwa kila la kheri na anaamini kuwa atarudi tena kuwa pamoja nao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.