Ligi Kuu

Polisi: JKT hawapati kitu.

Sambaza....

Baada ya timu ya Polisi Tanzania kuwadhibiti vilivyo wananchi wa Lindi na kuweza kuondoka na ushindi katika uwanja wa ugenini wa Majaliwa Ruhangwa mkoani Lindi sasa watahamishia makali yake katika uwanja wa wake wa nyumbani.

Tovuti ya Kandanda.co.tz imezungumza na Afisa Habari wa klabu ya Polisi Tanzania Frank Lukwaro na kujinasibu kuendeleza vipigo huku wakijiandaa kutoa burudani kwa mashabiki wake ambao tangu msimu huu uanze hawajaiona timu yao na pia hawajawaona wachezaji wao wapya.

Kikosi cha Polisi Tanzania kilipokua njiani kutoka Lindi kuelekea Moshi-Kilimanajaro

Frank Lukwaro ” Mchezo huu ni mkubwa sana kwetu  mashabiki wetu wametusibiri muda mrefu kuiona timu, tunawakaribisha mashabiki waje kuishuhudia. Tunajua mashabiki wameimiss sana timu na kuna baadhi ya wachezaji wapya ambao hawajawaona.

Kikubwa mchezo utakua mzuri lakini ni kwamba JKT Tanzania wajue hawachomozi na aina yoyote ya alama katika uwanja wetu wa Ushirika Moshi. Sisi tumejipanga kwa kushirikiana na mashabiki wetu.”

Baada ya ushindi wa bao moja bila dhidi ya Namungo ugenini Polisi Tanzania waataikaribisha Jkt Tanzania waliotoka kupokea kipigo cha bao mbili katika uwanja wa Jamuhuri Dodoma dhidi ya majirani zao Dodoma jiji fc. Mchezo huo utapigwa Ijumaa September 18 saa nane mchana.

Sambaza....