Sambaza....

Mwanakandanda mashuhuri Ronaldo de Assís Moreira maarufu kama Ronaldinho anatarajia kuoa wanawake wawili kwa pamoja katika jumba lake la kifahari huko Brazil kwa mujibu wa mirror.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan ameripotiwa kuwa anafunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Priscilla Coelho pamoja na mpenzi wake mpya ambaye wameanza kutoka wote Mwezi Agosti mwaka jana Beatriz Souza.

Inaelezwa kwamba Wanawake hao wawili wanaishi kwa amani wakiwa pamoja na staa huyo katika Jumba lake linalokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 13 lililopo Rio de Janeiro tangu Disemba mwaka jana.

Taarifa zimeendelea kusema kuwa wanawake wote wamepewa alawansi ya shilingi Milioni 4 kutumia watakavyo, pamoja na kununuliwa zawadi zinazofanana kama marashi wanapokuwa wamesafiri pamoja.

Ronaldinho aliwachumbia Wanawake hao kwa pamoja mwezi January pamoja na kuwavalisha pete ya uchumba, hii ni kwa mujibu wa mtu wake wa karibu Leo Diaz.

Atawaoa Wanawake hao kwa pamoja katika sherehe ndogo itakayofanyika Santa Monica katika mtaa wa Barra da Tijuca mjini Rio ambapo amekuwa akiishi tangu mwaka 2015.

Sambaza....