Sambaza....

Klabu ya soka ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imepeleka ombi Kwa bodi ya Ligi Kuu kutaka mechi za Nyumbani zinazozihusisha vilabu vya Simba na Yanga kufanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema baada ya kuona ombi la JKT Tanzania kukubaliwa mechi zao kupigwa CCM Mkwakwani wameona na wao wana haki kuchagua uwanja Kwa ajili ya mechi za Simba na Yanga.

Amesema wamefanya hivyo si kwamba wanaogopa kucheza Katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam bali ni kwasababu wapenzi wengi wa Ruvu Shooting wamewaomba kupeleka burudani hiyo mkoani Dodoma.

“Sio kwamba tunaogopa kucheza Kwenye uwanja wa Taifa, kuna mashabiki wengi wa Ruvu Shooting waliopo mkoa wa Dodoma wanatamani kuona burudani hii ya soka, naamini Bodi ya Ligi watakubaliana na hili na watatupa uwanja wa Jamhuri kuchezea mechi zetu,” Masau amesema.

Ruvu Shooting watacheza na Simba mwishoni mwa juma hili jijini Dar es Salaam hivyo Kama ombi lao litakubaliwa basi inawezekana mechi yao ikapigwa Katika Dimba la Jamhuri mkoani Dodoma.

Sambaza....