Ligi

SABABU Kwanini FRAGA ni bora kuzidi KOTEI

Sambaza....

Jana kulikuwa na mechi kati ya Simba na KMC katika uwanja wa uhuru , mechi ambayo tulishuhudia Simba wakishinda goli 2-0, magoli yaliyofungwa na Deo Kanda pamoja na Greson Fraga, ushindi huo umewafanya Simba wafikishe alama 31 wakiwa kileleni.

Katika mechi hiyo tumeendelea kushuhudia kiwango bora cha kiungo mkabaji Greson Fraga akifunga magoli mawili katika mechi mbili alizocheza hivi karibuni , Greson Fraga alikuja baada ya kuondoka James Kotei , zifuatazo ni sababu ambazo zinaonesha kwanini Fraga ni bora kuzidi James Kotei.

 

Kotei (Kushoto)

 

HAITAJI KUCHEZA “DOUBLE PIVOT”

Moja ya madhaifu makubwa ya James Kotei ni kucheza SINGLE PIVOT “acheze kiungo wa Kati mbele ya mabeki na viungo wa Kati “. Hawezi kucheza mwenyewe kwa sababu James Kotei anauwezo mzuri Wa kukaba na uwezo mdogo wa kusambaza mipira.

Udhaifu wake ni uwezo mdogo wa kusambaza mipira uwanjani , ndiyo maana kocha Patrick Aussems alikuwa anatumia DOUBLE PIVOT , James Kotei na Jonas Mkude, Jonas Mkude alikuwa anaziba madhaifu ya James Kotei ya kusambaza mpira , Kila James Kotei alipokuwa anakaba, Jonas Mkude alikuwa anachukua mipira na kusambaza.

Hiki kitu hakipo kwa Greson Fraga hahitaji kucheza Double Pivot kuonekana bora, yeye anauwezo wa kucheza katikati ya mabeki na viungo huku akipokonya mipira na kusambaza kulia, kushoto na mbele tena kwa usahihi.

KUPIGA PASI NDEFU NA FUPI

Greson Fraga anauwezo mkubwa kuzidi James Kotei katika kupiga pasi ndefu na fupi kwa ufasaha ndani ya mechi.

KUTAMBUA MIJONGEO YA WACHEZAJI WENZAKE

Uwezo wa Greson Fraga hauishii kwenye upigaji wa pasi pekee , pia uwezo na Kutambua mijongeo (movements ) za wachezaji wenzake na kuwapigia pasi kulingana na minjongeo husika.

KUCHEZA MPIRA KATIKA PRESHA KUBWA

Ukitamzama Greson Fraga anapopokea mpira huwa hana hofu hata kama anapokea mpira akiwa mbele ya wachezaji pinzani. Ana uwezo wa kutulia bila presha na kutoa pasi kwa wachezaji wenzake, hii kitu haipo kwa James Kotei kwa sababu kila anapokuwa anapokea mpira mbele ya wachezaji pinzani eneo ambalo hayuko huru huwa anashindwa kustahimili na kupoteza mipira.

Gerson Fraga Vieira

Kwa hiyo Greson Fraga amekuja kuongeza kitu ambacho awali hakikuwepo , Simba walikuwa wanatumia sana viungo wawili wa kukaba , kwa hiyo kuwa na Greson Fraga hakukulazimishi utumie viungo wawili wa kukaba kwa sababu anauwezo wa kupokonya mipira na kupiga pasi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.