Matola
ASFC

Safari ya Yanga mwisho kwa Lipuli

Sambaza....

Afisa habari wa Lipuli FC , bwana Clement Sanga amesema kuwa mwisho wa Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho ni kwenye uwanja wa Samora.

Akizungumza na mtandao huu wa Kandanda.co.tz amedai kuwa kuna watu wanadai Lipuli walibahatisha kuifunga Yanga katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Haruna Shamte akipiga mpira

Lipuli waliifunga Yanga kwa goli moja kwa bila katika uwanja wa Samora. Na lipuli wamefanikiwa kuingia katika hatua ya nusu ya fainali ya kombe la shirikisho baada ya kuifunga Singinda United.

Yanga na Lipuli watakutana katika hatua ya nusu fainali baada ya Yanga kuitoa Alliance Schools kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Yanga wakishangilia baada ya kuifunga Alliance Fc

Mchezo mwingine wa nusu fainali katika kombe hili la shirikisho itawakutanisha KMC na Azam FC. Azam FC waliitoa Kagera Sugar kwa goli moja kwa bila na KMC waliwatoa mabingwa watetezi Mtibwa Sugar.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x