Uhamisho

Samatta: Ilikua ni ndoto!

Sambaza....

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” baada ya kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa Aston Villa ya England ametoa ya moyoni baada ya kukamilisha dili hilo.

Baada ya kusubiri kwa siku kadhaa kukamilika kwa dili hilo hatimae jana usiku Aston Villa ilimtambulisha kua mshambuliaji wao mpya huku kocha Smith akiamini Samatta atawakoa katika janga la kushuka daraja. Villa ipo katika nafasi ya 18 ikiwa na alama 22 katika michezo 23 walioshuka dimbani.

Mbwana Samata akiitumikia KRC Genk katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

Baada ya kufanikisha usajili huo Samata alisema “Ilikua ni ndoto asante Aston Villa kufanya iwe kweli. Sasa ni muda wa kujitoa asilimia 100 kwaajili ya timu (Aston Villa).

Ndugu Watanzania nawashukuru kwa maombi yenu, mapambano yanaendelea. Haina kufeli!”

Mbwana Samatta pia alidokeza alikua akimfwatilia Gabriel Agbolanhor alipokua akiitumikia klabu hiyo iliyopo jiji la Birmingham huku wapinzani wao wakubwa wakiwa ni West Bromwich Albion na Birmigham City.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.