Blog

Sikuwa na furaha Simba- SENZO

Sambaza....

Moja kitu ambacho kilikuwa kinauliziwa na watu wengi sababu kubwa kwanini Senzo Mbatha aliamua kujiudhuru ndani ya klabu ya Simba.

Baada ya kutua rasmi kwenye ardhi ya Tanzania aliyewahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Simba , Senzo Mbatha ametoa sababu rasmi ya yeye kuondoka katika klabu ya Simba.

“Ulikuwa uamuzi mgumu sana na ulichukua muda mrefu , haukuwa uamuzi wa ndani ya siku moja tu. Ulikuwa uamuzi ambao ulichukua muda mrefu sana kuuchukua”.

“Wakati nachukua uamuzi huu nilikuwa nawaza kwenda nyumbani tu sikuwaza kwenda Yanga , lakini sijui Yanga walipatia wapi habari zangu za kuondoka na ndiyo wakanifuata”.

” Ila kusema ukweli Mimi sikuwa na furaha ndani ya Simba kuna vitu ambavyo nilikuwa naviona haviendi sawa na walikuwa Hawaii tayari kuvipokea”.

“Hata wewe mwandishi huwezi kufanya kazi sehemu ambayo hauna furaha. Hivi ndivo ilivyokuwa kwangu. Sikuwa na furaha na siwezi kufanya kazi sehemu ambayo sikuwa na furaha”.

“Sijutii uamuzi wangu . Nasonga mbele hata siku moja sijutii uamuzi wangu kwa sababu nilikaa chini na kutafakari kwa muda mrefu”- alimalizia Senzo Mbatha


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.