Kikosi cha Simba kikiwa mazoezini
Ligi Kuu

Simba balaa yashinda mechi mbili kwa siku moja

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imecheze michezo miwili ya kirafiki katika uwanja wa Uhuru na kuibuka na ushindi katika michezo yote hiyo ambayo ilifanyika majira ya asubuhi.

Mchezo wa kwanza ulikua ni kati ya Simba dhidi ya KMC ambapo Simba ilishinda mabao matatu kwa moja huku magoli yakifunga na Clatous Chama, Ibrahim Ajib na Mzamiru Yassin. Huku goli pekee la KMC likifungwa na Reliant Lusajo.

Kikosi cha kwanza kilikua hivi:

1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Kenedy Juma
5. Joash Onyango
6. Jonas Mkude
7. Mzamiru Yassin
8. Clatous Chama
9. John Bocco
10. Ibrahim Ajib
11. Miraj Athuman

Baada ya kupata ushindi mbele ya KMC na mchezo huo kumalizika Simba iliingia tena uwanjani kucheza na Transit Camp katika mchezo wa pili wa kirafiki.

Katika mchezo dhidi ya Transit Simba ilipata ushindi wa mabao matano kwa mawili. Magoli ya Simba yalifungwa na Gadiel Michael, Meddie Kagere, Charles Ilanfia na Kipenye aliefunga mawili.

Kikosi cha timu ya pili kilikua

1. Benno kakolanya
2. Kameta Duchu
3. Gadiel Michael
4. Ibrahim Ame
5. Erasto Nyoni
6. Said Ndemla
7. Kipenye
8. Larry Bwalya
9. Kagere
10. Charles Ilanfia
11. Morrison

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.