Tetesi

Simba kumtambulisha Streka Mcongo leo!

Sambaza....

Baada ya kumshusha Lary Bwalya kutoka Power Dynamos kutoka Power Dynamos kutoka Zambia Simba leo pia wana jambo leo katika kuendeleza  vuguvugu la usajili.

Cris Mugalu ambae nae pia anatokea Zambia anatajwa kutambulishwa leo na Wekundu wa Msimbazi Simba. Mugali anaecheza eneo la ushambuliaji anakwenda kuungana na kina John Bocco na Meddie Kagere kuongeza nguvu kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mugalu Cris.

Kabla ya kuitumikia Lusaka Dynamos Cris Mugalu ambae ni raia wa Congo alikua Green Eagles ya Zambia katika msimu wa 2018 kabla ya mwaka 2019 kujiunga na Lusaka Dynamos.

Kandanda inafahamu mshambuliaji huyo alitua nchini jana na Ethiopia Airlines pamoja na kiungo mpya Lary Bwalya ambae yeye alitambulishwa jana.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.