Wachezaji wa Simba wakishangilia mbele ya mashabiki wao
Ligi Kuu

Simba kuanza kutest mitambo!

Sambaza....

Baada ya takribani wiki mbili kuingia kambini  kuanza mazoezi ili kujiandaa na kurejea kwa Ligi Wekundu wa Msimbazi  Simba sc leo watacheza mchezo wa kirafiki  ili kujipima kabla ya kufungua dimba dhidi ya Ruvu Shooting.

Klabu ya Simba itaikaribisha KMC “Kino Boys” katika uwanja wao wa Mo-Simba Arena uliopo Bunju jijini Dar es salaam ili kujipima nguvu huku kocha wa Simba akipanga kutumia wachezaji wake wote waliopo kambini kasoro wachezaji wawili tu.

Simba itamkosa Sharaf Shiboub ambae bado yupo Sudan kwao na pia itamkosa Clatous Chama ambae amewasili nchini jana alitokea Zambia hivyo hatokua sehemu ya mchezo.

KMC imetoka kuifunga mabao matatu kwa bila klabu ya Yanga walipocheza pia mchezo wa kirafiki jana Jumapili katika dimba la Uhuru. Magoli ya KMC yalifungwa na Charles Illanfia, Hassan Kabunda na kiraka Sadala Lipangile.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.