Blessings Nkor mshambuliaji wa Yanga akimuacha mlinzi wa Simba
Ligi Kuu

Simba na Yanga kinawaka leo Uhuru.

Sambaza....

Ligi kuu ya Wanawake imeendelea kushika kasi ikiwa imeanza mzunguko wa pili kwa kasi mno huku vigogo Simba Queens na Yanga Princess wakipambania nafasi zao kivyao.

Tayari Ligi hiyo imefikisha michezo kumi na moja na leo michezo mingine itaendelea huku mchezo wa siku ukiwa ni kati ya wenyeji Yanga Princess wakiwakaribisha vinara wa Ligi Simba Queens.

 

Mchezo huo utapigwa leo majira ya saa kumi jioni katika Uwanja wa Uhuru ambapo katika mchezo wa kwanza ambao Simba walikua nyumbani uliisha kwa sare ya bao moja kwa moja.

Simba anaingia uwanjani akiwa kinara wa Ligi kwa alama zake 26 sawa na Fountain Gate Princess  lakini Simba wao wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Yanga wao wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 21.

Michezo mingine itakayopigwa leo katika Ligi hiyo Baobab Queens watawakaribisha  JKT Queens, Amani Queens watacheza na Ceasiaa Queens, Mkwawa Queens watawakaribisha Fountain Gate Princess na Alliance Girs watakua nyumbani dhidi ya The Tiger Queens.

Mchezo huo wa watani wa jadi unatarajiwa kuwa wa kuvutia kutokana na ushindani uliopo baina yao na matokeo ya sare katika raundi ya kwanza.

Lakini pia mchezo huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wadau wengi wa soka nchini kutokana na muda wa mechi lakini pia ushindani wa kiasili uliopo baina ya Simba na Yanga.

 

Sambaza....