ASFC

SIMBA ndiyo Baba lao, yaifunika YANGA

Sambaza....

Leo Simba imeonesha kuwa ndiyo baba lao Baada ya kuifunga Arusha United kwenye uwanja wa Uhuru , uwanja ambao jana ulitumika kwenye mechi dhidi ya Yanga na Iringa United.

 

Kwenye mechi ya Jana Yanga wakifanikiwa kushinda kwa magoli matatu ( 4) kwa bila (0) , huku magoli matatu (3 ) yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza , na goli la nne (4) likipatikana katika kipindi cha pili.

Leo hii Simba imevunja kilichofanywa na Yanga jana Baada ya kuifunga Arusha United kwa magoli sita (6) kwa bila , huku kipindi cha kwanza wakifanikiwa kufunga magoli namna (4).

Magoli ya Simba yamefungwa na Chama ambaye amefunga goli lake la pili la mashindano msimu huu, Gerson Fraga, Ibrahim Ajib ambaye amefunga goli lake la kwanza la mashindano , Deo Kanda , Francis Kahata na Meddie Kagere wamefanikiwa kufunga magoli mengine na kukamilisha idadi ya magoli kuwa sita (6).


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.