Yusuph Mhilu akishangilia baada ya kufunga goli lake katika mchezo dhidi ya Azam fc.
Blog

Simba njooni mnisajili – MHILU

Sambaza....

Kwa sasa inaonekana Meddie Kagere ndiye mwenye nafasi kubwa ya kubeba kiatu cha ufungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara akiwa na magoli 19 huku mtu anayemfuata ni Yusuph Mhilu mwenye magoli 13.

Msimu huu Yusuph Mhilu amekuwa na msimu mzuri sana , mpaka sasa hivi amefanikiwa kufunga magoli 16 huku akitoa pasi 4 za mwisho za magoli , akiwa amehusika kwenye magoli 20 mpaka sasa hivi .

Kiwango hiki kimemfanya kuwa ni mmoja ya wachezaji lulu ambao watagombaniwa kwa kiasi kikubwa kwenye dirisha kubwa la usajili kwa sababu ya timu nyingi zinaweza kumtaka.

Yusuph Mhilu (Kagera) akizidi kumtoka Makame (Yanga)

Yusuph Mhilu mkataba wake na Kagera Sugar unamalizika mwishoni mwa msimu huu hivo kumfanya awe mchezaji huru , Yusuph Mhilu amefanya mazungumzo na mtandao huu wa kandanda.co.tz

Katika mazungumzo hayo amedai kuwa yuko tayari kusajiliwa timu yoyote cha muhimu dau liwe zuri , hata kama ni Simba yeye anachoangalia ni dau tu ambalo litamuondoa Kagera Sugar.

“Kagera Sugar nawapa nafasi kubwa sana kwa sababu ni waajiri wangu , lakini kama Kuna timu yoyote ambayo inaweza kufikia dau langu basi nitakuwa tayari kujiunga na klabu hiyo”- alisema Yusuph Mhilu .

Yusuph Mhilu alipewa nafasi kwa mara ya kwanza na George Lwandamina kwenye kikosi cha Yanga kabla ya kuachwa na yeye kutimkia katika klabu ya Kagera Sugar aliyopo kwa sasa.

Sambaza....