Sambaza....

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club kinatarajiwa kuwasiri jijini Dar es Salaam leo Jioni kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya watani zao Dar Young Africans Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu.

Simba ambao wametoka kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui hapo jana wameondoka Shinyanga baada ya kufanya mazoezi asubuhi kuelekea Mwanza na baadae kusafiri hadi Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo.

“Asubuhi ya Leo tulifanya mazoezi hapa Shinyanga, tunashukuru kila kitu kipo sawa na Mungu akijaalia leo jioni tutakuwa Dar es Salaam “Abbas Suleiman Alli, ambaye Meneja na Mratibu wa Simba amesema.

Inasemakana baada ya kufika Dar kikosi hicho kitaelekea moja kwa moja Visiwani Zanzibar kuweka kambi ya siku chache kabla ya kwenda kuwavaa watani zao hao, huku Yanga wao ikisemakana wapo mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo.

Sambaza....