Ligi Kuu

Tamu na chungu za dakika ya mwisho!

Sambaza....

Hatimaye ligi kuu ya NBC imetamatika jioni ya leo na kukamilisha msimu wa 2021 -22
kwa Yanga African kutwaa ubingwa. Huku waliokuwa mabingwa watetezi Simba Sports wakimaliza kwenye nafasi ya pili.

Azam FC wana lambalamba wakimaliza kwenye nafasi ya 3 ya msimamo baada ya kuwafunga Biashara United 4-1 na kuwashusha daraja.

Matokeo ambayo yanaifanya Biashara United kuungana na Mbeya kwanza kuwa wameshuka rasmi na msimu wa pili watacheza championship.

Tanzania Prisons na Mtibwa sugar wao watakutana kucheza Play off itakayomnusuru moja wao kwenda kucheza hatua ya pili ya play off dhidi ya JKT Tanzania kwa upande wa ambaye ni mshindi toka Championship.

Ligi kwa ujumla ilikuwa ngumu na yeye kusisimua licha ya bingwa kupatikana mapema lakini kiwango cha ushindani kilikuwa kikubwa hadi dakika ya mwisho.

Na ndiyo maana timu za kushuka zimeanza kujulikana angalau kwenye round ya 29 ambayo ni Mbeya kwanza na kwenye siku ya mwisho Biashara naye akaporomoka.

Hapa inapaswa kuwapongeza sana wadhamini haswa wa haki za matangazo ya Television yaliochangia kuifanya ligi kuwa ngumu kwa sababu ya fedha watakazozitoa ni kutokana na nafasi uliyomaliza nayo tofauti na misimu mingine.

Hivyo basi michezo yote 240 ilikuwa na ushindani wa hali ya juu sana kila timu ikitaka kumaliza kwenye nafasi nzuri ipate mzigo (fedha ) ya maana.

Utofauti mkubwa na msimu uliopita mechi zilikuwa 306 kutokana na uwepo wa timu 18 lakini msimu huu ilikuwa na timu 16 tu.

George Mpole ameibuka mfungaji bora kwa kufunga goli 17 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Fiston Mayele aliyemaliza na goli 16.

Mpole anatoa tafsiri ya tofauti kwenye eneo la mfungaji bora ukifananisha na yule wa msimu uliopita John Bocco ambapo ligi ilikuwa na michezo 34.

Hata kinara wa assist msimu uliopita Clatous Chama 15 akifuatiwa na Luis Miquissone 10 Idd Nado 9 na wengineo.

Msimu huu ni tofauti sana Reliant Lusajo ameongoza akiwa na assist 6 akifuatiwa na akina Sakho wenye 5. Nachoweza kusema ligi ya msimu huu ilikuwa shindani sana sana tofauti na msimu uliopita.

Waamuzi nao kwa nafasi yao wamejitahidi sana walikuwa na makosa ya kibinadamu tofauti na msimu mwingine ambayo inaaminika kulikuwa na makosa ya makusudi kutokana na kutikulipwa stahiki zao.

Nimalizie kwa kuipongeza Bodi ya Ligi na TFF kwa kusimamia na kumalizika salama licha ya changamoto ndogondogo zilizoonekana katika msimu mzima.

Sambaza....