ASFC

TFF yaongeza waamuzi mechi ya Simba

Sambaza....

Baada ya sintofahamu kutokana na maamuzi mbalimbali ya marefa wetu hapa nchini TFF imeamua kuongeza idadi ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup.

Mchezo utakaopigwa leo kati ya Azam fc na Simba utachezeshwa na kusimamiwa na waamuzi saba.  Katika mchezo huo wa robo fainali ya nne utakuwa na mwamuzi wa kati, waamuzi wawili wa pembeni na pamoja waamuzi wa pembeni ya goli.

Waamuzi wataochezesha mchezo wa leo kati ya Azam fc na Simba sc.

Mchezo wa leo utatanguliwa na mchezo wa kwanza kati ya Sahare All-Star na Ndanda fc  ambapo mshindi wa hapo atakwenda kucheza na Namungl fc katika nusu fainali ya kwanza.

Mshindi kati ya Azam fc na Simba atakwenda kukutana na Yanga sc katika nusu fainali ya pili ya michuano ya Azam Sports Federation Cup.

Sambaza....