Blog

This Is Simba hakuanzisha Manara, nilianzisha mimi – Antonio Nugaz

Sambaza....

 

Vita ya maneno inazidi kuendelea kati ya Afisa habari wa Simba , Haji Manara na Afisa Mhamasishaji wa Yanga , Antonio Nugaz katika mitandao ya kijamii hapa nchini.

Akizungumza kwenye mtandao wa Instagram Mubashara na Ally Kamwe mchambuzi wa Azam Media , Afisa Mhamasishaji huyo wa Yanga amedai kuwa msemo wa This Is Simba alianzisha yeye na siyo Manara.

“Wakati nafanya matangazo yao mimi ndiye nilikuwa naingiza ile sauti kwa sauti iliyojaa huku nikisema (This Is Simba , ladies and Gentlemen ). Kwa hiyo mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kuisema tena kwa kunionesha” alimalizia Afisa Mhamasishaji huyo wa Yanga.

Alipoulizwa kama Haji Manara ana mchango kwenye mpira wetu , Antonio Nugaz alidai kuwa kwa kiasi kikubwa Haji Manara amejitajidi sana na anamchango mkubwa kwenye mpira wetu .

Haji Manara msemaji wa klabu ya Simba

 

“Mnyonge mnyongoni haki yake mpeni, kusema kweli Haji Manara amejitajidi sana kwenye mpira wetu hapa nchini , amejitajidi kujenga brand (chapa) yake , kuimarisha brand (chapa) ya Simba pia . Ana mchango mkubwa sana kwenye mpira wetu ingawa anatabia ya ujivuni sana” alimalizia Afisa Mhamasishaji huyo wa klabu ya Yanga SC.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.