Sambaza....

Winga machachari Uhuru Selemani Mwambungu ameiacha klabu yake ya Biashara United ya Mara na kutimkia tena Africa Kusini alikuwepo awali kabla ya kurudi nchini na kujiunga tena na Ligi Kuu Bara.

Uhuru Selemani “Luis Nani” amejiunga na klabu ya Royal Eagles inayoshiri ligi daraja la kwanza nchini Afrika ya Kusini. Uhuru amesaini kandarasi ya mwaka mmoja huku akionekana ni kama amerudi nyumbani baada ya kuwepo hapo misimh iliyopita.

Uhuru Selemani akiwa na vifaa vipya vya timu yake mpya.

Uhuru selemani amewashukuru viongozi wa Biashata united kwa kuweza kumruhusu kuinga tena na Royal Eagles huku pia akitoa shukrani za dhati kwa mashabiki wa Biashara United.

Uhuru Selemani amepitia vilabu mbalimbali vikubwa nchini kama Simba Sc, Coastal Union na Azam fc, pia akipata bahati ya kuitwa mara kadhaa kuitwa katika timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.

Sambaza....