ASFC

Usichokijua katika safari ya Simba kombe la FA!

Sambaza....

Nusu fainali ya AzamSports Federation Cup itapigwa Jijini Mwanza katika Dimba la CCM Kirumba kwa kuwakutanisha Watani wa Jadi Simba na Yanga May 28 mwaka huu.

Katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla utaamua ni nani atakwenda fainali kukutana na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Coastal Union na Azam Fc na kukutana fainali itakayopigwa July 2 Sheikh Amri Abeid Arusha.

Thadeo Lwanga akifunga bao mbele ya walinzi wa Yanga katika fainali ya Kombe la FA Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Kuelekea nusu fainali hiyo Wekundu wa Msimbazi wamejitengenezea historia ya aina yake mpaka kufikia katika nusu fainali kucheza na watani wao Yanga.

Simba mpaka kufikia hatua hiyo si tu imeshinda michezo yote lakini pia haijafungwa hata bao moja katika michuano hiyo baada ya kucheza michezo minne. 

Cris Mugalu akipiga shuti na kufunga mbele ya walinzi wa Dar City.

Ilianza kuifunga bao moja bila JKT Tanzania, halafu ikaipa kichapo kizito Dar City cha mabao sita kwa bila. Wakafwata Ruvu Shootinga wakafungwa saba kwa sifuri kabla ya kuivurumisha Pamba Fc mabao manne kwa bila na kutinga nusu fainali.

Rekodi nyingine waliyoiweka Simba msimu huu katika michuano hiyo ni kucheza michezo yake yote ya kombe hilo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Clatous Chama akipongezana na John Bocco baada ya kufunga bao katika mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting.

Simba imecheza michezo mitatu ikiwa mwenyeji dhidi ya Dar City, JKT Tanzania na Pamba Fc, halafu ikacheza ugenini dhidi ya Ruvu Shooting lakini Ruvu wakitumia Uwanja huohuo pia.

Hivyo basi kuelekea nusu fainali itakayopigwa Mwanza ndio mchezo pekee ambao Simba watacheza wakiwa nje ya Dar es salaam msimu huu katika kombe la FA.

Tayari Simba ipo Mwanza kitambo kujiandaa na mchezo huo wa nusu fainali ambao Simba ndio bingwa mtetezi wa kombe hilo.

Sambaza....