Ligi Kuu

Utamu umerudi mwanangu

Sambaza....

Ndioo ilee raha na uhondo wa soka letu umerudi tena na kivumbi kinaanza kutimka leo katika viwanja mbalimbali nchini huku michezo hiyo ikiwa mubashara kupitia Azam tv.

Msimu wa 2020/2021 wa Ligi Kuu Bara ambao inashirikisha timu 18 unakwenda kufungulia leo hii ambapo timu 12 zitashuka katika viwanja mbalimbali kuashiria ufunguzi wa Ligi pendwa na maarufu Afrika Mashariki na Kati.

Klabu za Ihefu, Gwambina na Dodoma fc ambazo kwa mara ya kwanza zinacheza Ligi Kuu Bara watashuka dimbani kuonja ladha ya Ligi Kuu. Ihefu wao watakua wenyeji wa Simba katika dimba la Sokoine, Gwambina watakua ugenini dhidi ya Biashara United wakati Dodoma Jiji wao watakua wanaikaribisha Mwadui fc.

Kesho pia kutakua na michezo mitatu ambapo KMC watacheza dhidi ya Mbeya City katika dimba la Uhuru, Azam fc wataikaribisha Polisi Tanzania Kagera Sugar wataumana na Jkt Tanzania.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.