Sambaza....

Kuelekea katika mchezo wao wa nne wa ligi kuu Bara dhidi ya Mbao utakaopigwa katika dimba la CCM Kirumba uongozi wa klabu hiyo umetoa kauli nzito kuelekea kwa wachezaji na mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi Simba.

Kuelekea mchezo huo wa leo msemaji wa Klabu ya Simba Hajji Manara amesema “Tumewaambia wachezaji kinachohitajika leo na wameahidi furaha kwa Wanasimba.”

Pia aliwapa neno neno mashabiki wa klabu yake “Mashabiki endeleeni kutuunga mkono na kutuombea. Always Simba ni moja na tutabaki hvyo. Tukishinda ni Simba na vyovyote vile ni Simba. Inshaalla tutashinda”

Ikumbukwe Simba wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbuu ya kutoka sare ya bila kufungana na Ndanda fc ya Mtwara katika dimba la Nangw’anda Sijaona.

Sambaza....