Benard Morrison
Tetesi

Yanga kuachana na Bernard Morrison?

Sambaza kwa marafiki....

Taarifa za ndani ya klabu ya Yanga zinadai kuwa katika ile orodha ya wachezaji watakaoachwa na klabu ya Yanga na jina la Bernard Morrison lipo.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya karibu vinadai kuwa Yanga wameamua kuachana na Bernard Morrison kutokana na utovu wake wa nidhamu ambao amekuwa akiuonesha.

“Kuna utovu mkubwa wa nidhamu ambao amekuwa akiuonesha ndani ya klabu kwa hiyo viongozi kwa pamoja wamefikia maamuzi ya kuachana naye”- kilisema chanzo chetu.

Kikosi kilichoaanza dhidi ya Kagera Sugar

Chanzo hicho kilizidi kuarifu mtandao huu kuwa Bernard Morrison amekuwa akionekana kama ni mkubwa kuliko klabu yenyewe ambayo ameikuta.

“Tatizo limeanza kwake yeye pia kuonesha kuwa ni mkubwa kuzidi klabu. Klabu ina miaka mingi kuzidi yeye na kaikuta ila anataka aonekane yeye ni mkubwa kuzidi klabu”- kilimazilia kusema chanzo chetu

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.