Jesus Moloko wa Yanga akimtoka mlinzi wa Simba Mohamed Hussein "Tshabalal"
Mabingwa Afrika

Yanga Sudan, Simba Kusini.

Sambaza....

Ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kwa hatua za awali tayari imetoka na vigogo Simba na Yanga tayari wameshawajua wapinzani wao.

Yanga wataanza hatua ya awali dhidi ya mabingwa wa Sudan Kusini Zaalan Fc ugenini na kisha wakishinda watakutana na mshindi kati ya Al Hilal ya Sudan au St. George ya Ethiopia.

Simba wao wataanzia ugenini dhidi ya Big Bullets ya Malawi na kumalizia nyumbani. Endapo Simba itafanikiwa kusonga mbele watakutana na mshindi kati ya Red Arrows ya Zambia au De Agosto ya Angola.

Kwa upande wa Geita Gold katika kombe la Shirikisho wao watacheza dhidi ya Al-Sahil ya Sudan Kusini halafu mshindi kati yao atacheza na Pyramids ya Misri.

 

Michezo yote hiyo ya Ligi ya Mabingwa itachezwa kati ya September 9 na 11 na micjezo ya marudiani itapigwa kati ya September 16 na 18 mwaka huu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.