Blog

YANGA wanatakiwa kuizidi SIMBA kumsajili KOTEI

Sambaza....

James Kotei anaonekana kuwa katika wakati mgumu Baada ya timu yake ya Kaizer Chiefs kuachana naye . Kuachana na mchezaji huyo kunamfanya awe huru kusajiliwa na timu yoyote kwa makubaliano binafsi.

Kuna Habari Simba inaweza ikamrudisha James Kotei Baada ya kuachana naye msimu huu, James Kotei alikuwa nguzo muhimu kwenye kikosi cha Simba msimu uliopita. Lakini James Kotei anahitajika zaidi Yanga na siyo Simba , sababu zifuatazo zinaonesha kwanini Yanga inamhitaji zaidi James Kotei.

HAWANA KIUNGO WA KUZUIA

Tangu msimu uliopita Faisal Fei Toto alihamishwa kutoka kwenye eneo la kiungo la ushambuliaji mpaka kwenye eneo la kiungo wa kuzuia. Hii ilitokana na Yanga kutokuwa na viungo wa kuzuia. Hii ilikuwa msimu jana.

Msimu huu Mwinyi Zahera Baada ya kushindwa kumtumia Patrick Tshishinbi kwenye eneo la kuzuia aliamua kumtumia tena Faisal Fei Toto kwenye eneo hilo , Baada ya Mwinyi Zahera kuondoka, Boniface Mkwasa alianza kumtumia Ally Sonso kwenye eneo hili. Kwa hiyo eneo hili limekuwa halina mtu sahihi na maalumu.

UZOEFU

Kotei (Kushoto)

James Kotei ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kwenye ligi kuu Tanzania na kwenye mashindano ya kimataifa , msimu uliopita alifanikiwa kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika na klabu ya Simba.

UONGOZI

Yanga kwa sasa inakosa idadi kubwa ya wachezaji ambao wanasifa ya kuwa wachezaji viongozi. Kuwa na wachezaji wengi wenye karba ya uongozi unaifanya timu iwe na chachu kubwa ya kupigania ushindi kutokana na hamasa inayojengwa na viongozi hao ndani ya timu.

Hivo Yanga wanatakiwa kuhakikisha kumrudisha James Kotei na wamefanikiwa watakuwa wamepata mtu sahihi kwenye eneo hilo ambalo linawasumbua sana


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.